emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Huduma Zetu

FAHAMU UKWELI KUHUSU MATUMIZI YA META YA MAJI

Mteja anastahili kulipa bili inayotokana na matumizi yake halisi .Matumizi halisi ya mteja yanapimwa kupitia meta ya maji ambayo ni mali ya Mamlaka,wanalipa kutokana na matumizi yao halisi yanayopimwa kupitia Meter zao. Meta ya Maji humsaidia mteja kuweza kufuatilia na kudhibiti matumizi yake ya Maji .

1.Masharti ya kufungiwa meta (dira) ya maji:

• Kuanzia siku mteja atakapo fungiwa meter, meta hiyo itakuwa chini ya dhamana yake na anapaswa kuhakikisha Usalama wake.Endapo meta itaharibiwa au kupotea mteja atalazimika kulipa gharama ya ununuzi wa meta nyingine.

• Meta (dira) ya maji itafungwa na mafundi wa Mamlaka tu.

• Mteja haruhusiwi kuifungua,kuitengeneza ,kuihamisha mahali itakapofungwa au kuruhusu watoto ama mtu mwingine yeyota kuichezea.

• Ni kosa mteja au mtu yeyote ambaye si mtumishi wa mamlaka kufanya marekebisho yoyote katika meta ,na yeyote ataepatikana na kosa hilo atakatiwa maji ikifuatiwa na hatua nyingine za kisheria.

• Mteja atawajibika kusaini mkataba wa maandishi wakati wa kufungiwa meta ya maji.Mteja atapatiwa nakala ya mkataba huo na atapaswa kuutunza na kuutoa wakati wowote utakapohitajika.