Matangazo
TAARIFA KWA UMMA
Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) inapenda kuwataarifu wateja wake kuwa zoezi la usomaji wa Dira za Maji limeanza leo tarehe 20 Juni 2024.Mamlaka inaomba ushirikiano kwa Wananchi pindi watoa huduma wa GEUWASA watakapopita kutekeleza zoezi hili.
Mara baada ya kusomewa Dira ya Maji utapokea ujumbe mfupi (sms) katika simu yako wa kuhakiki usomaji katika Dira yako kabla ya bili kutumwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kwa namba 0800750060 bure au WhatsApp kwa namba 0754560565 (huduma kwa wateja GEUWASA).
“Geuwasa Maji yetu, Uhai Wetu”