Historia
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Geita (GEUWASA) iliundwa chini ya kifungu cha sheria ya maji na.8 ya mwaka 1997 sehemu ya 3(1) kama ilivyofanyiwa mabadiliko katika sheria na.5 ya mwaka 2019. GEUWASA likiwa ni shirika la Umma lilianza kazi rasmi tarehe 01 Julai 2012 likiwa na jukumu la kisheria la kusambaza Majisafi na kuondoa Majitaka katika Mji wa Geita.
Mamlaka ina Bodi ya Wakurugenzi walioteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Maji kwa ushauri wa Mkuu wa Mkoa. Bodi ina Wajumbe 10 wanaowakilisha makundi ya jamii kama ifuataavyo: Watumiaji maji wa nyumbani, Wafanyabiashara, Serikali ya Halmashauri ya Mji wa Geita, Madiwani, Wanawake na Wizara yenye dhamana na Sekta ya maji.
Mamlaka ilianzishwa kwa misingi ya kutoa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kibiashara katika misingi endelevu