emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Majukumu na Wajibu wa GEUWASA

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Geita (GEUWASA) iliundwa chini ya kifungu cha sheria ya maji na.8 ya mwaka 1997 sehemu ya 3(1) kama ilivyofanyiwa mabadiliko katika sheria na.12 ya mwaka 2009 sehemu ya 60. GEUWASA likiwa ni shirika Umma lilianza kazi rasmi tarehe 01 Julai 2012 likiwa na jukumu la kisheria la kusambaza majisafi na Usafi wa mazingira mjini Geita katika Manispaa ya Geita.

Mamlaka ina Bodi ya Wakurugenzi walioteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Maji kwa ushauri wa Mkuu wa Mkoa. Bodi ina Wajumbe 10 wanaowakilisha makundi ya jamii kama ifuataavyo: Watumiaji maji wa nyumbani, Wafanyabiashara, Serikali ya mji Mkuu na Manispaa, Madiwani, Wanawake na Wizara yenye dhamana na Sekta ya maji.

Mamlaka ilianzishwa kwa misingi ya kutoa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kibiashara katika misingi endelevu

MAJUKUMU NA WAJIBU WA GEUWASA

 • Kuhakikisha wateja wake wanapata majisafi na salama.
 • Kuhakikisha kuwa uondoshaji wa majitaka kwa wateja wake unafanyika katika hali ya usalama.
 • Kuhakikisha upatikanaji wa fedha za kutosha ili kulipia Ankara ya umeme ya mitambo ya kusukuma maji uendeshaji wa ofisi, kulipa mishahara ya uendeshaji na matengeneso ya miundo mbinu na mifumo ya mabomba ya majisafi, usafi wamazingira na sehemu ya uwekezaji ili huduma hii iwafikie wakazi wengi wa Bukoba mjinii
 • Kuajiri watumishi waadilifu na wazalendo.
 • Kukusanya maduhuli yanayotokana na mauzo ya majisafi, huduma zamajitaka na ada mbalimbali zinazotokana na huduma hizo.
 • Kutosababisha usumbufu kwa mteja.
 • Kwa kushirikiana na wadau wengine, kusimamia utunzaji wa mazingira kwenye vyanzo vya maji.

HAKI ZA MAMLAKA

 • Kutobugudhiwa Mtumishi wake na mteja au chombo kingine wakati wa kutimiza wajibu wake.
 • Kushtaki au kushtakiwa pale ambapo haki haikutendeka.
 • Kulipwa malipo halali kutokana na huduma iliyotolewa kwa mteja.
 • Kusitisha huduma ya majisafi kwa mteja asiyetimiza wajibu wake au taratibu zilizowekwa mfano: kutolipia, kuchepusha maji au kuharibu mita ya maji.
 • Kuweka na kusoma dira ya maji kwa mteja wake kila mwezi mara mbili yaani tarehe 01-08 kila mwezi kwa utaratibu na ufuatiliaji wa matumzi ya maji na tarehe 13-19 ya kila mwezi ili kuandaa Ankara.
 • Ugawaji wa Ankara ni tarehe 25-31 ya kila mwezi.
 • Kufanya mabadiliko wakati wowote kwa mujibu wa sheria kadiri itakavyohitajika, mfano viwango vya malipo n.k.