emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Huduma Zetu

Maunganisho Mapya

Hatua za kufuata:

Mteja atajaza fomu ya maombi ya kuunganishiwa huduma ya maji.Fomu zinapatikana Jengo la huduma kwa wateja bila malipo yoyote fomu hiyo inaambatanishwa na nakala ya hati ya nyumba /kiwanja na ramani ya mtaa (site plan).

Wataalam wa mamlaka watafanya ukaguzi(survey kwenye eneo/nyumba inayoombewa huduma ya maji na kutayarisha gharama.

Mteja atapata taarifa ya ukaguzi na gharama za kuungiwa maji baada ya siku nne kuanzia tarehe aliyojaza fomu ya maombi ya huduma.Taarifa hizi atazipata kwenye madirisha ya huduma kwa wateja.

Gharama zote zinazohusika zitalipwa katika mamlaka na mteja atapewa risiti inayolingana na malipo atakayofanya.

TAHADHARI!! Mamlaka haitahusika na mapatano au malipo yoyote yatakayofanywa nje ya utaratibu uliowekwa na mamlaka.

2.Gharama zitakazohusika:-

Gharama za mabomba na viungio vinavyohitajika kuanzia bomba kuu hadi kufika katika eneo /la kiwanja cha mteja

Gharama za kuchimba na kufukia mtaro wa bomba.

Gharama za usimamizi (supervision charge)

Gharama za uwakala (agency fees-20%)

Ongezeko la thamani (VAT).

Endapo mteja atafanya malipo atastahili kupata huduma hiyo ndani ya siku nne kuanzia tarehe atakayokuwa amefanya malipo.

Iwapo kutakuwa na sababu zisizozuilika zitakazofanya mteja asipatiwe huduma katika muda uliopangwa ,Mamlaka itampa mteja taarifa rasmi.

Endapo mteja hatakuwa ameridhaika na huduma atakayopewa ana haki ya kuwasilisha maoni yake kwa Afisa Uhusiano

Ukiwa na maulizo yoyote kuhusu maelezo haya wasiliana na ofisi ya Uhusiano na wateja.