Habari
ZIARA YA KAMATI YA USALAMA WILAYA YA MBOGWE KWENYE MRADI WA MAJI MASUMBWE.
Kamati ya Usalama Wilaya ya Mbogwe ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe. Sakina Mohamed, imetembelea Mradi wa Uboreshaji wa Huduma ya Maji Masumbwe unaotekelezwa na GEUWASA.
Kamati hiyo imetembelea kilipo Chanzo cha Maji pamoja na eneo lilipo Tenki la kuhifadhia Maji lenye Ujazo wa lita 150,000.
Aidha Kamati hiyo imemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali Wakazi wa Mbogwe kwa Utekelezaji wake wa Miradi Mbalimbali Wilayani humo

