emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Habari

KIKAO CHA BODI KUU YA WAKURUGENZI ROBO YA TATU MWAKA WA FEDHA 2025/2026.


Leo tarehe 13 Mei 2026, kimefanyika kikao cha Bodi Kuu ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) katika ukumbi wa mikutano wa GEUWASA. Kikao hicho kimehusu tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo wajumbe wa bodi wamepata nafasi ya kujadili kwa kina mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za maji safi na usafi wa mazingira katika Mji wa Geita.