Habari
GEUWASA YAFANYA KIKAO KAZI CHA TATHMINI YA HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI WILAYANI MBOGWE.
Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) imefanya kikao kazi na Madiwani pamoja na Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Mbogwe katika maeneo inayowahudumia. Kikao hicho kililenga kufanya tathmini ya utoaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira pamoja na kusikiliza maoni, changamoto na mapendekezo kutoka kwa viongozi hao.
Katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa GEUWASA, Mhandisi Frank Changawa, alipokea na kujibu kero mbalimbali zilizowasilishwa na viongozi hao, sambamba na kuchukua hatua za haraka na dharura kwa baadhi ya maeneo yenye changamoto, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama. Pia alissitiza viongozi na wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha ......
Kwa upande wao viongozi walioshiriki kikao hicho pia waliipongeza GEUWASA kwa juhudi zinazoendelea kufanyika katika kuboresha huduma za maji pamoja na kupendekeza vikao hivyo vifanyike mara kwa mara ili kurahisisha na kuboresha huduma kwa wananchi.
GEUWASA inaendelea na dhamira yake ya kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora ya maji safi na salama kwa maendeleo ya jamii na uchumi.

