emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Habari

KIHONGOSI AFURAHISHWA NA USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI MZURI WA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 GEITA.


Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, ametembelea Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa katika Mji wa Geita kwa lengo la kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati. Katika ziara hiyo, Ndg. Kihongosi amepongeza juhudi za Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha zilizowezesha utekelezaji wa mradi huo wenye manufaa makubwa kwa wananchi wa Geita. Aidha ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) kwa usimamizi mzuri na utekelezaji wa mradi huo akieleza kuwa hatua hiyo ni chachu ya maendeleo na itasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya Majisafi na salama kwa wakazi wa Manispaa ya Geita pamoja na vijiji 19 vya Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Ndugu Kihongosi amesema mradi huo unaonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii huku akisisitiza wananchi kuendelea tutoa ushirikiano kwani kukamilika kwa mradi huo kuna manufaa makubwa ya kizazi cha sasa na kijacho.