Habari
MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJI COMPAUND
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) Mhandisi Frank Changawa akiambatana na Wataalamu wa GEUWASA pamoja na Mwenyekiti akiwa na Mtendaji wa Mtaa wa Compaund wametembelea eneo la Compaund ya juu ambalo lina changamoto ya ufikishaji wa huduma.
Lengo ikiwa ni kuboresha huduma ya MajiSafi kwa Wakazi wa maeneo hayo ya Mtaa hasa yaliyo juu.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Frank Changawa amewaomba Viongozi na Wakazi wa maeneo hayo kuendelea kutoa ushirikiano na kuwa wavuimilivu wakati Mamlaka ikiendelea na hatua mbalimbali za haraka za maboresho ya Miundombinu ya Maji ya maeneo hayo ili kuhakikisha Maji yanawafikia kwa wakati pindi yanapoelekezwa maeneo hayo.