Habari
KUNDO ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 GEITA.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo A. Mathew ametembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Miji 28 kwa Mji wa Geita kutoka katika Chanzo cha Maji cha Ziwa VIcktoria.
Mhandisi Kundo amefurahishwa na utekelezaji mzuri wa Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya AFCONS Infrastructure LTD kutoka nchini India.
Pamoja na kuridhishwa na utekelezaji wa Mradi huo Mhandisi Kundo amemtaka Mkandarasi kukamilisha kazi zote kabla ya muda wa mwisho wa mkataba.
Aidha Mhandisi Kundo ametoa wito kwa Wananchi wanaoishi karibu na Vyanzo vya Maji kutunza Vyanzo hivyo pamoja na miundombinu yake kwa kutambua kuwa Maji ni Uhai.

