emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Habari

Taarifa kwa Umma............................................


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA),Anapenda kuwa taarifu wateja na wadau wote wa GEUWASA kuibuka wimbi la utapeli kwa njia ya Mitandao ya Simu kuwataka wateja kutuma pesa ili kupatiwa huduma za Maji. GEUWASA inapenda kuwafahamisha Wateja na Wadau wote kuwa malipo ya huduma zote yanalipwa kwa kutumia kumbukumbu namba ya malipo (Control number) Hivyo ni kosa na hairuhusiwi kumpatia mtu yeyote fedha ili kupata huduma. Fanya malipo yako kwa kutumia ''Control number'' yako (inayoanza na 99408...) kupitia mitandao ya simu au Benki ya CRDB,NMB,NBC na AZANIA popote ulipo.