emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Habari

MABORESHO YA HUDUMA


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) Mhandisi Frank Changawa ameanza zoezi la ufuatiliaji wa maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Maji ambapo zoezi hilo limeanza katika Kampuni ya Bluecost Investment. Zoezi hili ni endelevu kwa maeneo yote yenye changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Maji ili kuona namna gani ya kuboresha miundombinu na kufikisha mtandao wa Maji kwa maeneo yote ambayo bado hayajafikiwa na mtandao.