Habari
KIKAO KAZI CHA UTEKELEZAJI WA MWAKA MPYA WA FEDHA
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) Mhandisi Frank Changawa,mapema leo tarehe 05/07/2024 amefanya Kikao Kazi kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mwaka mpya wa fedha kilichohusisha Menejimenti na Watumishi wote wa GEUWASA ikiwa ni sehemu ya kujengeana uwezo na kupeana maelekezo mbalimbali kwa ajili ya tija ya Mamlaka.