emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Habari

KAWAIDA ATEMBELEA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 GEITA.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg. Mohamed Kawaida ametembelea Mradi wa Maji wa Miji 28 Geita. Ndg. Kawaida akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wamepongeza hatua zinazoendelea katika Mradi huo unaogharimu Dola za Kimarekani Milioni 53.463 ambapo kukamilika kwake utaenda kumaliza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Maji kwa Halmashauri ya Manispaa ya Geita.