Habari
MKURUGENZI MTENDAJI WA GEUWASA AKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI BULELA - NYASEKE NA SHILOLELI
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafiri wa Mazingira Geita (GEUWASA) Mhandisi Frank Changawa ametembelea eneo la utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Bulela - Nyaseke na Shiloleli unaotekelezwa na Mkandarasi DS PERA LTD wenye thamani ya Tsh Million 445,191,481.91, ambapo kwa sasa umefikia asilimia 15 za utekelezaji.
Mhandisi Frank Changawa amefika kukagua shughuli zinazoendela kwasasa ambazo ni uchimbaji wa mshingi wa tanki lenye ujazo wa lita 135,000,Ujenzi wa nyumba ya pampu pamoja na ulazaji wa nguzo za umeme
Kukamilika kwa Mradi wa Maji Bulela - Nyaseke na Shiloleli utaenda kunufaisha Wakazi wasiopungua 13,313 wa Kata tatu za Bulela,Nyaseke pamoja na Shiloleli.