Habari
MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA GEITA (GEUWASA) IMETIA SAINI MKATABA WA MAKABIDHIANO YA MRADI WA MAJISAFI MANGA
Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) imetia saini Mkataba wa makabidhiano ya Mradi wa MajiSafi Manga Kata ya Mgusu Wilaya ya Geita kutoka kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Geita.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Meneja wa RUWASA Wilaya ya Geita Mhandisi Sande Batakanwa ambapo kwa GEUWASA Meneja huduma kwa wateja Ndugu Ashirafu Remtula ameshiriki kusaini Mkataba huo.
Kabla ya makabidhiano hayo ya Mradi wa MajiSafi katika Mtaa wa Manga lilifanyika zoezi la kuutembelea Mradi husika likiwahusisha Wataalam mbalimbali kutoka GEUWASA na RUWASA na Viongozi wa Mtaa wa Manga pamoja na Jumuiya ya Watumia Maji.