emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Habari

MKUU WA WILAYA YA GEITA AKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI BULELA - NYASEKE NA SHILOLELI.


Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe.Hashim Komba amefanya Ziara katika eneo la utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Bulela - Nyaseke na Shiloleli unaotekelezwa na Mkandarasi DS PERA LTD wenye thamani ya Tsh Million 445,191,481.91, ambapo kwa sasa umefikia asilimia 20 za utekelezaji. Shughuli zinazoendelea kwa sasa ni ujenzi wa Tanki lenye ujazo wa lita 135,000 ambapo kukamilika kwake kutanufaisha Wananchi wasiopungua 13,313 wa Kata za Bulela,Nyaseke pamoja na Shiloleli. Aidha Mhe.Hashim Komba amefurahishwa na jitihada za Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Geita ( GEUWASA ) pamoja na Mkandarasi kwa kasi iliyopo katika kuhakikisha Mradi huu unakamilika. “Mazingira ya Mradi ni magumu Tanki linajengwa juu ya Mlima na hakuna namna yoyote gari linaweza kufikisha vifaa vya ujenzi hapa,vifaa vinaishia chini na kubebwa na Mwanadamu kwenye kichwa,kwa mujibu wa taarifa Mradi ni wa miezi 7 kwahiyo nategemea Mradi ukamilike mwezi Novemba 2024 hivyo niwatake GEUWASA pamoja na Mkandarasi kutimiza malengo mliyojiwekea“ amesema Mhe.Hashim Komba.