emblem

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita
(GEUWASA)

Habari

MKUU WA WILAYA YA GEITA AMEISISITIZA MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA GEITA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI WA NYANKANGA KABLA YA MWEZI JULAI 2024.


Mhe:Hashim Komba amesema hayo katika ziara yake katika eneo la utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Utanuzi wa Mtambo wa Kutibu Maji Nyankanga ambapo amepata taarifa ya hali ya utekelezaji pamoja na taarifa ya uvunjwaji wa Mkataba na Mkandarasi GIPCO COMPANY LIMITED baada ya kusuasua kukamilisha mradi huo kinyume cha makubaliano. Meneja Usambazaji Maji katika Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA ) Mhandisi Isaack Mgeni alipokuwa akisoma taarifa hiyo ya utekelezaji ambapo ameelezea moja ya sabubu ya kuvunja Mkataba na Mkandarasi GIPCO COMPANY LIMITED ni baada ya kushindwa kutimiza majukumu yake ya kimkataba pamoja na kuongezewa muda. Mhe.komba ameisisitiza Mamlaka kufuata taratibu zote za usitishaji wa mkataba ili kuepuka Serikali kupata hasara ikiwa taratibu zitakiukwa “inami yetu mtaongeza msukumo mkubwa kwenye jambo hili ili mradi uweze kukamilika na hatimaye wananchi waweze kupata huduma ya maji” amesema Mhe.Hashim Komba. Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya TZS Bilioni 1.1 ambao awali ulipangwa kukamilika tarehe 31/05/2024,Mamlaka imepanga kukamilisha mradi huo kwa kutumia wataalam wa ndani na kukamilika kwa mradi huo kutapunguza adha ya upatikanaji wa huduma ya Maji wakati serikali ikiendelea kukamilisha mradi mkubwa wa maji wa Miji 28 kwa Mji wa Geita.